Tanzania Census 2022

📍SHIRIKA LA POSTA LAINGIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA BENKI YA EQUITY TANZANIA📍

SHIRIKA LA POSTA LAINGIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA BENKI YA EQUITY TANZANIA

Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Equity Tanzania limeingia makubaliano ya kibiashara yatakayoboresha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki nchini.

Makubaliano hayo yamefanyika leo tarehe 11 Novemba, 2021 mara baada ya Taasisi hizi mbili kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Daniel Mbodo amesema kuwa shirika la Posta lipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi hivyo makubaliano haya yatawezesha upatikanaji wa huduma za kibenki kote nchini hasa ikizingatiwa kuwa Posta ina mtandao mpana wenye matawi zaidi ya 322 Nchi nzima

“Tunajivunia kuweza kuungana na Benki ya Equity katika kufanikisha mpango huu utakaosaidia kufikisha huduma za kibenki kwa Watanzania wengi zaidi”. Alisema Mbodo.

Aliongeza kuwa,kwa sasa Shirika la Posta limejipanga na limeboresha utoaji wa huduma zake ambazo kwa sasa zinafanyika kidigitali kwani Shirika limeweka mifumo wezeshi kwa ajili ya utoaji wa huduma kwa haraka. Pia Shirika limeboresha mifumo ya usalama ili kuhakikisha usalama wa bidhaa za wananchi kwa kufunga CCTV kwenye ofisi zake nchini.

Tumejenga mifumo wezeshi kwa ajili ya utoaji huduma wa haraka pamoja na kufuatilia vitu vinachotumwa kupitia muundombinu wa posta hadi kuwafikiawateja. Tumeimarisha usalama kwa kufunga CCTV kwenye miundombinu yetu ili kila kinachopita posta kifike kwa usalama.

Bwana Mbodo aliongeza “Tunayo sababu ya kuwakaribisha na wengine wapate kile ambacho Benki ya Equity wamekifuata”, “Ukitaka kutoboa nchi nzima tumia POSTA

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania Ndg. Robert kiboti alisema kuwa Benki ya Equity inaendeshwa kwa sera ya kuwawezesha na kuwapatia wananchi huduma zilizo bora zaidi na nafuu ili kuweza kuwakomboa kiuchumi, ambapo mpaka hivi sasa kuna jumla ya mawakala 3,900. 

Hii itaongezea wigo wa utoaji huduma za kifedha na kuwakomboa watanzania kiuchumi kwa kuongeza ushiriki wa mfumo rasmi wa kifedha ambapo mahali popote penye Shirika la Posta patapatikana huduma za Benki ya Equity.

“Benki ya Equity ina jumla ya mawakala 3,900, hivyo kupitia Posta kama wakala mkuu wetu tunaweza kuongeza idadi ya wananchi watakaofikiwa na huduma zetu kwa ukaribu na urahisi zaidi”

Imetolewa na; 

Kitengo cha Mawasiliano 

Shirika la Posta Tanzania

11 Novemba,2021

7EC10EC6 CAB9 4EC7 AE5D 2EF31EEACA30

D4F936FE 2280 4FBE 9D16 E3389375C645

A15AF2D3 5DD7 4649 84D3 931228F0E8FE

D6677805 2F50 4A2B 9587 DEF63401EA57

C644DBB1 BB1A 4751 8B23 513B2EDFDE03

92BD52D0 915F 4ADD 8360 4F9044F9E18E

C2DC121B C155 44BF B337 0FF311B627EA

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!