📍KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI AKUTANA NA UONGOZI KUTOKA POSTA BURUNDI📍

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI AKUTANA NA UONGOZI KUTOKA POSTA BURUNDI

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula amepokea ujumbe kutoka Shirika la Posta Burundi ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bi. Lea Ngabire kwenye ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.

Ziara hiyo yenye lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya mawasiliano ya Posta imechagizwa na hatua iliyofikiwa na Shirika la Posta Tanzania ya kufanya mageuzi na maboresho makubwa ya mifumo ya uendeshaji wa Shirika la Posta nchini hasa katika eneo la Biashara mtandao ambapo Duka Mtandao la Posta limekuwa kivutio kwa nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) limelekea nchi nyingi kutaka kuja kujifunza kutoka Posta ya Tanzania.

Aidha, Bi. Lea Ngabire akiwa mkoani Dodoma  akiongozana  na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la  Posta Tanzania  walimtembelea Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba kwa lengo la kuendelea kujifunza huduma za Mawasilinao kwa wote zinavyowafikia wananchi wa maeneo ya vijijini.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano,

Shirika la Posta Tanzania.

19 Novemba, 2021

B44B5973 B5D8 4BE8 ABBC C8311BB50100

E2B8C73C 326D 4882 BEEF DBEEE0011235

948279E6 FBF0 41C3 B8D5 B718800EDA93

942BC095 16BF 4F86 B395 58B02D3EC5B5

FC072DD6 606C 4386 A64C C936F291A2F3PICHA NA MATUKIO WAGENI KUTOKA BURUNDI WALIPOTEMBELEA OFISI ZA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE (UCSAF)

E3A9CEF6 33B3 4993 9E97 7F1DB4389484

855A272A F685 4366 9DDB 1119FB94DA2F

6CAD63B9 1BF5 455A 9455 0D74839B92D1

2ECE1AF3 6CF4 4588 80A3 197C38599862

 

 

 

 

 

 

 

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!