📍POSTA NA MIKAKATI YA KUKUZA UCHUMI WA BULUU ZANZIBAR📍

POSTA NA MIKAKATI YA KUKUZA UCHUMI WA BULUU ZANZIBAR

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice mbodo leo ametoa wasilisho la Huduma za Shirika la Posta Tanzania mbele ya Baraza la Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika ukumbi wa mikutano wa Peoples Palace, Zanzibar.

Kikao hicho, kilichoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said, ambapo Kaimu Postamasta Mkuu alipata wasaa wa kuelezea Shirika lilipotoka, lilipo sasa na mwelekeo wake wa baadaye katika kuwezesha upatikanaji wa huduma bora zenye tija kwa Taifa na kuchangia ukuaji wa  uchumi wa Bluu Zanzibar.

Bw. Mbodo ameelezea Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika la Posta nchini zinazochochea  kukua  kwa uchumi wa buluu visiwani humo, ikiwemo huduma za usafirishaji, huduma ya Duka Mtandao la Posta, huduma za uuzaji na usambazaji wa stempu hasa zenye historia na vivutio mbalimbali vilivyopo visiwani Zanzibar.

Sambamba na hilo,Bwana Mbdodo alieleza kuwa, Shirika la Posta Tanzania linaendelea kuboresha huduma zake ili wananchi wa pande zote za Muungano waweze kunufaika na huduma hizo.

Wakati huo huo Bw. Mbodo ameliomba Baraza la Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuendelea kuhamasisha wananchi wa Zanzibar kutumia huduma za Posta ili kuchangia pato la Taifa na hatimaye kukuza uchumi wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla

Katika hatua nyingine, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta alipata nafasi adhimu ya kukabidhi Zawadi ya saa maalumu kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said yenye Nembo ya Shirika la Posta, picha za stempu zenye vivutio vilivyopo Zanzibar, picha ya magari kuonesha huduma ya usafirishaji, na Duka mtandao la Shirika ikiwa ni sehemu ya huduma za Shirika la Posta zenye lengo la kukuza maendeleo ya uchumi wa buluu Zanzibar. 

Kaimu Postamasta Mkuu aliambatana na Meneja mkaazi Zanzibar Bw. Ahmad Mohamed Rashid, Meneja Barua na usafirishaji Bw.Jasson Kalile,  pamoja na viongozi waandamizi wa Shirika hilo.

 

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano;

Shirika la Posta Tanzania.

23 Novemba, 2021.

 

9A063555 45AA 4DB1 9F48 C4E89EB3DD03

C5712901 B0D0 4AA7 A3E2 790CDFAB3DF8

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Daniel Mbodo (Kulia) akielezea picha mbalimbali za stempu zilizopo kwenye saa hiyo

48D395B1 CC4B 4071 B5AE 62CEE64895E1

5985A14A F835 45B9 817B B23D5F4514E0

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Daniel Mbodo (Kulia) akikabidhi saa maalum kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said (kushoto)

389D176A FCBD 4087 AF16 24C0D236F444

Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said (kushoto) akiifurahia saa maalum aliyokabidhiwa kama zawadi na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Daniel Mbodo (Kulia)

 

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!