📍POSTA KUTANGAZA HUDUMA ZAKE KUPITIA MPOTO📍

POSTA KUTANGAZA HUDUMA ZAKE KUPITIA MPOTO

  •    Mrisho Mpoto kuwa Balozi wa  Shirika la Posta
  •     Ujumbe kutoka Umoja waPosta Duniani (UPU)    
        watarajiwa kuja nchini

 

SHIRIKA la Posta Tanzania limeingia makubaliano kati yake na msanii wa nyimbo na Mshairi Bwana  Mrisho Mpoto maarufu 'Mjomba' kuwa balozi wa Posta kwa lengo la kutangaza huduma na bidhaa za Shirika ambalo lipo katika mageuzi makubwa katika utoaji huduma ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla iliyoambatana na utiaji saini wa makubaliano hayo Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Macrice Daniel Mbodo amesema, lengo la kuingia makubaliano hayo ni kulitangaza Shirika la Posta ambalo lipo katika mabadiliko makubwa ya kulitoa kwenye analojia kuwa Shirika la kidigitali katika utoaji huduma.

''Makubaliano haya ni kwa ajili ya kulitangaza Shirika letu la Umma ambalo kwa sasa linaenda kidigitali na sio shirika la barua kama wengi wanavyodhaani.  Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika yapo jijini Arusha hapa Tanzania hii nafasi adhimu kwetu kuonesha kuwa tulistahili kuletewa makao makuu haya kwa kufanya  mageuzi ya haraka na yenye tija kwa uchumi wa taifa na tunawahimiza wananchi kutumia huduma za Posta kama nchi nyingine wanavyofanya.'' Amesema.

Mbodo amesema, Shirika la Posta lina fursa nyingi ambazo jamii inatakiwa kuzifahamu na kuzitumia ikiwemo huduma ya Duka Mtandao ambayo huwezesha kuuza na kununua bidhaa kwa njia ya mtandao kote duniani.

''Posta ina miundombinu ya usafirishaji ndani na nje ya nchi tunasafirisha hadi samaki na dagaa kupeleka nje ya nchi tutumie fursa hii, pia kuna huduma za kifedha zinazotolewa katika shirika hili, Vituo vya Huduma Pamoja (One Stop Centre) zinapatikana katika ofisi za Posta kwa mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma hivyo ni vyema wananchi wakatumia fursa hizo kupitia Shirika lao.'' Amesema.

Wakati huo huo, Kaimu Postamasta Mkuu, amesema kuwa Shirika la Posta linaendelea kuimarika vyema na wanategemea kupokea ujumbe kutoka Umoja wa Posta Duniani (UPU) ambapo Tanzania ni mwanachama hai wa Umoja huo.

''Kupitia balozi mteule Mpoto, watanzania watapata fursa ya kulifahamu Shirika la Posta  na huduma zinazotolewa kwa uaminifu na gharama nafuu, ni juzi tu Shirika la Posta ( Royal Mail) ya Uingereza ilitushirikisha katika kusafirisha kifimbo cha Malkia kwenda nje ya nchi, kama wenzetu walivyotuamini nami niwaombe watanzania wenzangu tuunge mkono na kutuamini katika juhudi za Serikali kupitia Shirika letu la Posta.'' Amesema.

Kwa upande wake balozi mteule Mrisho Mpoto ameshukuru kwa kupewa nafasi hiyo na kuwashauri watanzania kupenda na kuthamini vitu vya nyumbani ili waheshimiwe duniani na kukuza kipato na soko.

Mpoto amesema shirika la Posta ni la kidijitali, salama na wanamtandao mkubwa wa usafirishaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi na kuahidi kuwafikia watanzania wengi na kuwafahamisha juu ya huduma na bidhaa za Shirika hilo zenye uhakika na viwango vya kimataifa.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano;

Shirika la Posta Tanzania.

25 Novemba, 2021.

 

191E2630 8670 4464 9988 767D19D79D9D

1C96577C 482B 4FC4 813A 2C95F9E86331

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo (kulia) pamoja na Balozi mpya wa Shirika la Posta Tanzania, Mshahiri Mrisho Mpoto wakisaini hati za makubaliano mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla fupi ya kumtambulisha Balozi huyo, iliyofanyika katika Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Dar es salaam

BF9AA347 F732 4FDF 983A BFDDBF3D6614

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo (kulia) akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumtambulisha Balozi wa Posta, Mshahiri Mrisho Mpoto (kushoto), iliyofanyika katika Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Dar es salaam 

C5702E9B 39C0 4378 A04E 1A616F4504B9

Balozi mpya wa Shirika la Posta Tanzania, Mshahiri Mrisho Mpoto (kushoto), akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo Bw. Macrice Mbodo

9ADA8392 F2A7 4E11 8B76 12965DAE01D1

11DD0B9C 44AA 4696 A3D5 90CDC407B374

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo (kulia aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika la Posta nchini, mara baada ya hafla. Kulia aliyekaa ni Balozi mpya wa Shirika hilo Mshahiri Mrisho Mpoto

C8501EB5 F48D 4A8E B19E 933FD6B75B89

Mrisho Mpoto akiwa ofisini kwa Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta nchini Bw. Macrice Mbodo

1136AED8 BF39 4A94 8264 FAA5738AD7ED

Balozi mpya wa Shirika la Posta Tanzania, Mshahiri Mrisho Mpoto (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Makao Makuu ya Shirika la Posta, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo Bw. Macrice Mbodo

4884F63B 023B 422F 939C 60DDAE2B4D47

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!