Tanzania Census 2022

📍 POSTA YASHIRIKI KONGAMANO LA 12 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI 📍

POSTA YASHIRIKI KONGAMANO LA 12 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI

📍AICC, Arusha📍

Shirika la Posta Tanzania ambalo ni miongoni mwa wadhamini wa Kongamano la 12 la mwaka la Wataalam wa Manunuzi na Ugavi nchini limeshiriki Kongamano hili leo tarehe 2 Disemba, 2021 linalofanyika kwenye Ukumbi wa AICC jijini Arusha.

Shirika la Posta Tanzania limetumia jukwaa hilo kufanya wasilisho juu ya huduma na biashara mbalimbali zinazofanya na Shirika hilo hapa nchini. Wasilisho hilo limefanywa na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara za Shirika Bwana Constantine Kasese kwa niaba ya Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo Bwana Macrice Daniel Mbodo.

Bwana Kasese ameelezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika la Posta nchini ikiwemo huduma za Usafirishaji wa barua na vipeto, huduma za Uwakala na Fedha ikiwemo “Bureau de Change”, EMS pamoja na huduma nyingine nyingi.

Aidha Bwana Kasese ametumia jukwaa hilo kuelezea huduma mbalimbali zilizoboreshwa na Shirika hasa huduma za kidijitali ikiwemo huduma ya Duka Mtandao (Posta Online Shop) ambalo linawapa fursa wajasiriamali nchini na hata nje ya nchi kutangaza na kuuza bidhaa zao kupitia duka hilo lililounganishwa na nchi zaidi ya 192 zilizopo chini ya Umoja wa Posta Duniani (UPU) na hata kuwezesha watu wengi duniani kuagiza na kununua bidhaa popote walipo duniani.

Aliendelea kueleza kuwa huduma za kidijitali zilizoanzishwa na Shirika ni pamoja na huduma ya Posta Kiganjani (SmartPosta) inayomuwezesha mteja kufuatilia taarifa ya mzigo au barua anayotuma akiwa popote pale alipo. Alisema kuwa huduma hii inapatikana kwa kupakua “application” ya “SmartPosta” inayopatikana “Play Store” na baada ya hapo mtumiaji ataweza kujisajili ili kuanza kuitumia huduma hiyo.

Sambamba na hilo Bwana Kasese aliongeza kuwa Shirika la Posta nchini limeanzisha vituo vya “Huduma Pamoja” vinavyotoa huduma mbalimbali za Serikali katika ofisi za posta ambapo kwa awamu ya kwanza Shirika limeanzisha vituo hivyo kwenye mikoa wa Dar es Salaam na Dodoma.

Huduma zinazopatikana kwenye vituo hivyo ni pamoja na huduma za NSSF, PSSF, RITA, NIDA, BRELLA, TRA, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CRDB na NHIF.


Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania,
2 Disemba, 2021

5D40FD09 30E3 4F67 86BF 485DE3A482D4

28279124 95AC 4ADD A344 1F1AC29CA6E7

A9B95610 415F 4ED7 8C83 9705D39AC579

Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara Bw. Conastantine Kasese akiwasilisha wakati wa Kongamano hilo

D90FD704 949A 4A82 BD89 8FD7443A82B3

3D1DC618 BB74 45AB 9488 739E92DE1E4F

B6859C46 A658 4677 A9D1 BAC629BE1E31

C6CB42F9 B51F 497C 82D5 E211CBB203E1

ECBED20C 89C0 42A9 8EC6 8CCA98144F0D

Baadhi ya watumishi wa Shirika la Posta wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa Kongamano hilo

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!