POSTA YASHIRIKI UZINDUZI WA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI JIJINI MWANZA.

POSTA YASHIRIKI UZINDUZI WA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI JIJINI MWANZA.
 
IMG 20211203 WA0063
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo (kulia) akikabidhi zawadi ya Shirika hilo kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) wakati wa maonesho ya kimataifa ya wajasiriamali kwenye viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza.
 
 
 
Na Mwandishi Wetu,  Mwanza
 
Shirika la Posta Tanzania likiongozwa na Kaimu Postamasta Mkuu, Ndugu Macrice Daniel Mbodo limeshiriki Uzinduzi wa matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Posti Kodi kwa Mkoa wa Mwanza.
 
Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 3 Disemba 2021 katika Viwanja vya shule ya Msingi Buhongwa Jijini Mwanza, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi nchini kwa mwaka 2022, Mhe. Anna Makinda. 
 
 
Wakati wa Uzinduzi huo, Kamisaa  Makinda aliainisha jinsi mfumo huo unaotumia simu ya mkononi na vifaa vingine vya kielektroniki utakavyorahisisha maisha ya wananchi katika upatikanaji wa huduma muhimu za kiuchumi na kijamii bila usumbufu na kuwafikia mahali walipo.
 
 
Katika maelezo yake Mhe. Makinda aligusia namna mfumo huu utakavyonufaisha watumiaji wa huduma za posta nchini ambapo, itakuwa rahisi kwao kufikiwa mpaka walipo pindi watakaposafirishiwa barua,vipeto na vifurushi vyao. "Kupitia anwani zenu za makazi, hata posta watapata urahisi wa kutoa huduma za kusafirisha mizigo yenu na barua zenu" alisisitiza Mhe. Makinda.
 
 
Uzinduzi huo, ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi, na  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula(Mb).
 
Mara baada ya Uzinduzi huo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi, walipata wasaa wa kutembelea mabanda  mbalimbali ya maonesho ya 21 ya Kitaifa ya wajasiriamali wa chini na wa Kati katika Viwanja vya "Rock City Mall"  likiwemo Banda la Shirika la Posta,
 
Akiwa katika banda la Shirika la Posta Tanzania Mheshimiwa Dkt Kijaji alijionea mageuzi makubwa ya utoaji huduma yaliyofanywa na Shirika, huduma mbalimbali za kidijitali zinazotolewa na Shirika la Posta kwa kutumia fursa ya maendeleo ya teknolojia ambazo zimerahisishwa na hivyo kuwapa wananchi wanachokihitaji. Akiwa bandani hapo Mhe Dkt Kijaji alikabidhiwa zawadi na Kaimu Postamasta Mkuu Bwana Macrice Mbodo.
 
Aidha, maonesho hayo yanayoendelea Jijini Mwanza yamehudhuriwa na nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na South Sudan.
 
 
 
Imetolewa na 
Ofisi ya Mawasiliano 
Shirika la Posta Tanzania.
 
 
 
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO. 
 IMG 20211203 WA0021
Mgeni Rasmi, Uzinduzi wa matumizi ya Mfumo wa anwani za makazi na Postikodi kwa Mkoa wa Mwanza, ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022, Mhe. Anna Makinda.
 
 
 IMG 20211203 WA0065
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akimsikiliza na Kaimu Postamasta Mkuu, Ndugu Macrice Mbodo (kulia), mara baada ya kuwasili kwenye Banda la Shirika la Posta kwenye maonesho ya kimataifa ya wajasiriamali, katika viwanja wa Rock City Mall, Jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Katibu Makuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi (kushoto).
 
 
 
 
 IMG 20211203 WA0060
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo (kulia) akikabidhi zawadi ya Shirika hilo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (kushoto). Katikati ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
 
 
 
 IMG 20211203 WA0026
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndugu Macrice Mbodo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa ubora TCRA Ndugu Haruni Lemanya (kushoto), wakati walipohudhuria Uzinduzi wa Mfumo wa anwani za makazi na Postikodi Jijini Mwanza.
 
 
 IMG 20211203 WA0067
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akisaini kitabu cha wageni katika Banda la Shirika la Posta, kwenye uwanja wa Rock City Mall wakati wa maonesho ya kimataifa ya wajasiriamali, Jijini Mwanza.
 
 
 
 
 IMG 20211203 WA0019
 
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania Mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja mbele ya banda la Shirika hilo, wakati wa maonesho ya kimataifa ya wajasiriamali, kwenye uwanja wa Rock City Mall jijini Mwanza.
 
 
 PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO...
 IMG 20211203 WA0069
 
 
IMG 20211203 WA0024
 
 
IMG 20211203 WA0025
 
 
 IMG 20211203 WA0030
 
 
 IMG 20211203 WA0027
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!