POSTA YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA WAJASIRIAMALI.

POSTA YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA WAJASIRIAMALI.
 
 
 IMG 20211208 WA0003
 
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Mwanza wakiwa tayari kuhudumia wateja. 
 
 
Na Mwandishi Wetu,  Mwanza
 
Shirika la Posta Tanzania linashiriki Maonesho ya 21 ya Wajasiriamali wadogo na wa kati wa Afrika Mashariki maarufu kama maonesho ya Nguvu Kazi /Jua Kali yanayofanyika katika viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza. 
 
 
Maonesho haya yalianzishwa kwa lengo la kuwaunganisha wajasiriamali wa Afrika Mashariki ili kubadilishana ujuzi na mbinu mbalimbali za kibiashara. Kwa mwaka huu maonesho haya yanafanyika nchini Tanzania katika Jiji la Mwanza huku yakibeba kauli mbiu isemayo "Kuhamasisha ubora na uvumbuzi, ili kuongeza ushindani wa wafanyabiashara wadogo na wakati wa Afrika Mashariki na kuinuka kiuchumi baada ya janga la UVIKO-19".
 
Shirika la Posta Tanzania imeshiriki maonesho haya kwa kutangaza na kutoa huduma zake mbalimbali hasa za Duka mtandao, Posta kiganjani pamoja na huduma za Usafirishaji.
 
 
Maonesho hayo yamehudhuriwa na nchi mbalimbali za Afrika Mashariki zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan ya Kusini na Tanzania mwenyewe.
 
 
 Imetolewa na 
Ofisi ya Mawasiliano 
Shirika la Posta Tanzania.
 
 
PICHA MBALIMBALI ZA MAOMESHO HAYO
 
IMG 20211210 WA0051
 
 
IMG 20211210 WA0052
 
BeautyPlus 20211211124425836 save
 
 
IMG 20211207 WA0066
 
 
IMG 20211208 WA0003
 
 
 
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!