POSTA YATOA SEMINA ELEKEZI KWA MAMLAKA YA UDHIBITI WA MBOLEA TANZANIA (TFRA).
Shirika la Posta Tanzania kupitia Idara ya Masoko leo imefanya Semina elekezi kwa baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo iliyolenga kueleza huduma za Shirika la Posta imeendeshwa na Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Masoko, Ndugu Andrea Liundi, Meneja Biashara Mtandao wa Shirika la Posta Tanzania, Mhandisi Fifi Kulwa na Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Barua Bi lightness Mushi.
Imetolewa na
Ofisi ya Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania.
PICHA NA MAELEZO.
Mkurugenzi wa huduma za Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Bi. Victoria Elangwa (kulia) akipokea zawadi mbalimbali za Shirika la Posta Tanzania kutoka kwa Afisa Mwandamizi idara ya Barua kutoka Shirika la Posta Tanzania , Bi. Lightness Mushi (kushoto).
Kaimu Meneja Rasilimali watu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Bi. Naomi Fwemula (katika) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Posta Tanzania.
Afisa Masoko Mwandamizi kutoka Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Andrea Liundi akitoa semina elekezi juu ya huduma za Shirika la Posta kwa baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).
Meneja Biashara Mtandao wa Shirika la Posta Tanzania, Mhandisi Fifi Kulwa akitoa ufafanuzi wakati wa semina elekezi juu ya huduma za Shirika la Posta Tanzania kwa baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).
Afisa Mwandamizi idara ya Barua kutoka Shirika la Posta Tanzania , Bi. Lightness Mushi akisisitiza jambo wakati wa semina elekezi iliyotolewa na Shirika la Posta kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).