SHIRIKA LA POSTA LAJIDHATITI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA USAFIRISHAJI.

SHIRIKA LA POSTA LAJIDHATITI  KUBORESHA MIUNDOMBINU YA USAFIRISHAJI. 
 
IMG 20220205 132252 585
 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese (kushoto) akikabishi Gari kwa Meneja wa Posta Mkoa wa Shinyanga Bw.Julius Mponda(kulia)  ikiwa ni Jitihada za Shirika la Posta kuongeza vitendea kazi vya usafirishaji katika Mikoa mbalimbali ya Nchini.
 
 
 
 
Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeendelea kuboresha utoaji huduma kwa wateja wake kwa kuongeza vitendea kazi vya usafirishaji katika mikoa mbalimbali ya nchini ili kuleta ufanisi  kwenye kuihudimia jamii. 
 
Vitendea kazi hivyo vya usafirishaji vimetolewa na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese pamoja na Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika Bw. Samwel Aron ambao kwa pamoja wameendelea kukabidhi magari kwa Mikoa mbalimbali kwa niaba ya Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Bw. Macrice Mbodo. 
 
Mikoa iliyopokea vitendea kazi hivyo ni pamoja na Morogoro, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Mzizima. Pia Zanzibar, Dar es salaam, Mwanza, Kigoma na Shinyanga vimepokea magari hayo kwa lengo la kuboresha utendaji na kuongeza ufanisi hasa kwenye eneo la Usambazaji.
 
Kuongeza vitendea kazi muhimu ikiwemo magari mapya, vifaa vya ofisi na rasilimali watu, kutaboresha ufanisi, kasi na weledi katika kutoa huduma ni sehemu ya maheuzi makubwa ya kulifanya Shirika hili kuwa jukwaa muhimu la kuchangia ukuaji wa uchumi jamii kwenye mabadiliko ya teknolojia. Shirika linajipambanua katika nyanja ya usafirishaji na matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma ulioshuhudia maboresho mbalimbali yaliyofanywa na Shirika hilo hivi karibuni ikiwemo ufunguzi wa Duka la Posta Mtandao na vituo vya  Huduma Pamoja vinavyohusisha watoa huduma za kiserikali mahala pamoja ndani ya ofisi za Posta.
 
Akizungumza wakati wa kuhitimisha zoezi hilo Kaimu Meneja Mkuu, Uendeshaji wa Biashara Bwana Constantine Kasese amewaasa madereva watakaokabidhiwa magari hayo kuyatunza vizuri ili yalete tija kwa Shirika na Wananchi na yaweze kudumu kwa kuwa yatarahisisha usafirishwaji wa vifurushi na nyaraka za wateja kwa masaa 24 katika mikoa yote Nchini.
 
Imetolewa na: 
Ofisi ya Mawasiliano 
Shirika la Posta Tanzania
 
 
 
PICHA NA MAELEZO:
 IMG 20220205 132252 600
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese (kulia) akikabishi Gari kwa Meneja wa Posta Mkoa wa Mwanza, Bw. Dongwe James Dongwe (kushoto) ikiwa ni Jitihada za Shirika la Posta kuongeza vitendea kazi vya usafirishaji katika Mikoa mbalimbali ya Nchini.
 
 
IMG 20220205 132252 604 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese (kushoto mwenye kaunda suti ya bluu) akikabishi Gari kwa Meneja wa Posta Mkoa wa Kigoma, Bw. Phillip Mchele (kulia aliyekaa ndani ya gari) ikiwa ni Jitihada za Shirika la Posta kuongeza vitendea kazi vya usafirishaji katika Mikoa mbalimbali ya Nchini.
 
BeautyPlus 20220204160952689 save 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese(kulia mwenye kaunda suti ya kahawia) akiwa kwenye picha ya wafanyakazi wa Posta Mkoani mwanza, mara baada ya kukabidhi gari litakalofanya kazi ya usafirishaji na usambazaji wa nyaraka, barua na vifurushi vya wateja Mkoani humo.
 
 
BeautyPlus 20220204164337058 save 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese(katikati mwenye kaunda suti ya bluu) akiwa kwenye picha ya wafanyakazi wa Posta Mkoani Kigoma.
 
 
BeautyPlus 20220204164607129 save 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese( mwenye kaunda suti ya bluu) akisoma hati ya Gari kwa Meneja wa Posta Mkoa wa Kigoma Bw. Phillip Mchele (kulia).
 
 
IMG 20220205 132252 648 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese (suti ya bluu) akiwa kwenye kikao cha makabidhiano ya gari Mkoani Shinyanga. Aliyesimama ni Meneja wa Posta Mkoa wa Shinyanga Bw.Julius Mponda.
 
 
IMG 20220205 132252 644 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese (kushoto mwenye kaunda suti ya bluu) akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa Dagaa na Samaki Mkoani Kigoma.
 
IMG 20220205 132252 615 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wa Dagaa na Samaki Mkoani Kigoma, Wakati alipowatembelea na kufanya mazungumzo tarehe 3 Februari mwaka huu. 
 
 
BeautyPlus 20220204165558808 save
 
 
 
BeautyPlus 20220204165349923 save
 
 
BeautyPlus 20220204165247829 save 
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!