POSTA YASHIRIKI KIKAO KAZI CHA WAKUU WA MIKOA KUHUSU ANWANI ZA MAKAZI.

POSTA YASHIRIKI KIKAO KAZI CHA WAKUU WA MIKOA KUHUSU ANWANI ZA MAKAZI.
 Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa nchini, kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi, tarehe 8 Februari 2022, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
 
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa nchini, kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
 
Kikao kazi hicho kimefanyika leo tarehe 08 Februari, 2022 huku kikihudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Kitaifa, Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja na Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani.
 
Katika kikao hicho,  Rais Samia amewataka Wakuu wa Mikoa kutekeleza zoezi la kukamilisha Anwani za Makazi kwa kipindi cha miezi mitatu hadi mwezi Mei mwaka huu, huku akieleza faida zitakazopatikana katika mradi huo ikiwemo, wafanyabiashara na wajasiriamali wanaofanya biashara mtandao kutambulika kwa urahisi mahali walipo na kutambua wateja wao mahali walipo. 
 
Aidha alieleza kuwa, kupitia mradi wa Anwani za Makazi, usafirishaji wa nyaraka, vifurushi na mizigo mbalimbali itawafikia kwa urahisi kupitia anwani za mitaa na nyumba zao huku akiongeza kuwa hata zoezi la Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, itafanyika kwa urahisi zaidi kupitia namba za nyumba na majina ya mitaa. 
 
Naye Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo ambaye ameshiriki kikao kazi hicho amezungumza baada ya kikao Kazi hicho kuwa Posta itaweza kuhudumia watanzania hadi walipo na pia kupitia duka mtandao la Posta wananchi wanaonunua bidhaa watazipata kupitia Muundo mbinu huo.
 
Itakumbukwa kuwa mfumo wa anwani za makazi ni suala lililojadiliwa na kuwekewa Maazimio na Umoja wa Posta Duniani (UPU) kupitia Mkutano wake Mkuu wa 25 uliofanyika mwaka 2012 mjini Doha ilitambua kuwa mtu asiye na Anwani ni mtu asiyekuwepo.
Pia Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003  inaelekeza kuwa Anwani za Makazi na Postkodi ziwekwe nchi nzima.
 
Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mfumo huu unakamilika katika kata na wadi 4174, Halmashauri 196 na Mikoa 31 Nchi nzima ifikapo Mei 2022.
 
Imetolewa na: 
Kitengo Cha Mawasiliano 
Shirika la Posta Tanzania
 
 
 
PICHA NA MAELEZO, 
 
IMG 20220208 WA0036 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania,  Bw.Macrice Daniel mbodo (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said(kushoto) wakati wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa nchini, kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi, tarehe 8 Februari 2022, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
 
IMG 20220208 WA0033
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake ,Jamii na Makundi Maalumu, Dkt Zainabu Chaula (kushoto) wakati wa kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa nchini kuhusu Anwani za Makazi jijini Dodoma leo.
 
 
IMG 20220208 222701 121 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Daniel Mbodo (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Channel Ten, Bwana Shaaban Kisu wakati wa kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Anwani za Makazi jijini Dodoma leo.
 
 
IMG 20220208 WA0030 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani Bwana Ramadhani  Kailima( kushoto) na Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma Bwana Ferdinand Kabyemela (kulia)wakati wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa nchini, kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi, tarehe 8 Februari 2022, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
 
 
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO: 
 
IMG 20220208 222701 133
 
 
IMG 20220208 222701 127
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!