SHIRIKA LA POSTA TANZANIA, LATOA MISAADA KWA WAZEE.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro.
Shirika la Posta Tanzania Mkoa wa Morogoro limetoa misaada mbalimbali ya kuukaribisha mwaka mpya katika kituo kinachotunza wazee kiitwacho Fungafunga kilichopo mkoani humo.
Misaada hiyo imetolewa na Meneja wa Posta Mkoa wa Morogoro Bi. Magreth Mlyomi, tarehe 5 Februari 2022, kama ilivyo desturi ya Shirika hilo kurudisha kwa jamii kile kilichopatikana kila mwanzo mwaka ikiwa ni ishara ya kuishukuru jamii kwa mchango wake kwa Shirika.
Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kituo hicho Bw. Ray Frida Ndomba amelishukuru Shirika la Posta Tanzania kwa kuwatembelea na kuwapa misaada hiyo na kuomba Mashirika mengine mbalimbali yaige mfano huo.
Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania.
PICHA ZAIDI.
Meneja wa Posta Mkoa wa Morogoro Magreth Mlyomi (kushoto aliyeinama) akikabidhi bidhaa mbalimbali alizopeleka katika kituo cha kutunza wazee cha Fungafunga kilichopo Mkoani Morogoro.