Tanzania Census 2022

📍MWENYEKITI WA BODI YA TPC AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA USIMAMIZI WA UBORA📍

MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA USIMAMIZI WA UBORA WA ISO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo leo tarehe 04 Aprili, 2022, amefungua rasmi mafunzo ya utekelezaji wa usimamizi wa ubora yaani ISO 9001:2015 kwa Menejimenti ya Shirika hilo mjini Morogoro

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo viongozi wa Shirika la Posta katika kuhakikisha wanatoa huduma zenye ubora na zenye tija kwa wananchi

Aidha, Brigedia Jenerali Mabongo ametumia nafasi hiyo kuitaka Menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha kila kinachofanyika katika utoaji wa huduma za Posta kiwe chenye ubora unaostahili na chenye tija kulingana na mahitaji ya wadau wote wa Shirika.

Kwa upande wa Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo amemuhakikishia Mwenyekiti wa Bodi hiyo kuwa kupitia mafunzo ya utekelezaji wa mfumo huo Shirika linaenda kutoa huduma zenye ubora zaidi ili kukidhi mahitaji ya wadau wake, kwani Shirika kupitia mpango mkakati wake wa 7 na wa 8 wa biashara iliweka lengo mahususi la kuhakilisha Shirika linapata cheti cha ubora wa kimataifa yaani ISO 9001:2015 hadi ifikapo June 2023

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Shirika la Posta Tanzania David Andrea ametumia nafasi hiyo kuushukuru uongozi wa Shirika hilo kwa kukubali na kuona umuhimu wa kuendesha mafunzo hayo katika Shirika kwani mafunzo hayo yataliwezesha Shirika kuongeza masoko na kurahisisha biashara baina ya nchi na nchi

 

 

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania.
04. 04. 2022.

 

 

PICHA NA MATUKIO

C83E17B5 ED5A 4F5A 8B8B 31E841526EB8

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo

 

7AB70AC5 BEC1 4D0F 8A58 9106B9FF176A

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo


8392377D 6CB0 4B7B BF17 CBFA0E294210

Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Shirika la Posta Tanzania David Andrea akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo Hayo

54771C41 111B 4C8B 9D1B 22E28AD342EC

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania wakifuatilia kwa makini ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo

35C3B2E6 A648 4597 B8A9 1AA0CDDCC6F0

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo

CA9443BE 5487 41A1 899B 8842B12B23E5

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti wa Shirika hilo, mara baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo

EC03D06D FF1B 4DB7 8D4B 76F84D607F35

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo akieleza jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo alipotembelea ofisi za Shirika la Posta mkoani Morogoro, mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo


MATUKIO MBALIMBALIMBALI WAKATI WA MAFUNZO HAYO

 

5FBE69C8 5998 49F9 A291 8CF30939A423

4593B573 55B0 4297 BE7F 921016BD47EB
CACCD9B2 07CC 486C 8C55 149E6AA9D85B

567BFFF0 3148 4EC8 B13C 90E72E815BA1

DCED241A FB73 4491 97AE 5A0D3C9B4D81

B395F815 E1CA 4938 9CD2 91D40460DD84

 

 

 

 

 

 

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!