POSTA KINARA KWENYE MAONESHO YA 5 YA MIFUKO NA PROGRAMU ZA KUWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI MJINI MOROGORO.

 
 
POSTA KINARA KWENYE MAONESHO YA 5 YA MIFUKO NA PROGRAMU ZA KUWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI MJINI MOROGORO.
IMG 20220516 WA0000 
 
 
Yakabidhiwa tuzo kwa kushika nafasi ya kwanza kundi la Taasisi za Serikali.
 
Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeshiriki kwenye maonesho ya tano ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi. Maonesho hayo yamefanyika kuanzia tarehe 9 hadi 14 Mei 2022 kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
 
Maonesho haya yalilenga zaidi kuonyesha kazi na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mifuko na Programu mbalimbali za kuwezesha wananchi kiuchumi na pia kuelimisha wananchi namna mifuko hiyo inavyowezesha wananchi na wajasiliamali kiuchumi kwa lengo la kuwajengea uwezo kiuchumi kwa kuwapatia mikopo na dhamana za kimtaji.
 
Maonesho haya yalifunguliwa rasmi tarehe 9 Mei na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martin Shigela kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda Dkt. Ashatu Kijaji.
 
Aidha Shirika la Posta Tanzania limeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye maonesho hayo kundi la taasisi za Serikali zilizoshiriki maonesho hayo na kujinyakulia Ngao na Cheti maalum cha ushindi. Ushindi huo umechagizwa zaidi na utoaji wa huduma zake kwa njia za kidijitali zilizoboreshwa na zinazoendana na mabadiliko ya kiteknolojia ikiwemo huduma za Duka la mtandaoni na Sanduku la Posta la kidijitali (Virtual Box).
 
Huduma hizi za kidijitali ndizo zilizovuta hisia na hamasa kwa wananchi waliotembelea banda la Posta na kupelekea kujiunga na huduma hizo za kisasa zinazotolewa la Shirika hilo.
 
Maonesho hayo yamehitimishwa leo tarehe 14 Mei, 2022 na Mhe. Dkt. Kijaji kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 
 
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania
14 Mei, 2022
 
 
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO: 
 
IMG 20220516 WA0010
 
 
IMG 20220516 WA0012
 
 
IMG 20220516 WA0011
 
 
IMG 20220516 WA0013
 
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!