TANZANIA YAONGOZA KIKAO CHA KAMATI NAMBA 2 YA BARAZA LA UENDESHAJI LA UMOJA WA POSTA DUNIANI (UPU).

 
 
TANZANIA YAONGOZA KIKAO CHA KAMATI NAMBA 2 YA BARAZA LA UENDESHAJI LA UMOJA WA POSTA DUNIANI (UPU).
 
 
 IMG 20220516 WA0003
 
Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Posta Duniani Bw. Mesahiko Metoki (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Constantine Kasese (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Kamati namba mbili ya Baraza la Uendeshaji la Umoja huo, wakati Kasese akiongoza vikao hivyo vinavyoendelea jijini Bern, Uswis.
 
 
Tanzania imeshiriki Mkutano wa Baraza la Uendeshaji la Umoja wa Posta duniani ulioanza tarehe 9-13 Mei, 2022 jijini Berne, Uswis. 
 
Katika Mkutano huo Tanzania imeongoza kikao cha Kamati namba 2 inayohusika na masuala ya Huduma za Posta na Biashara Mtandao (Physical services and E-commerce) ya Baraza la Uendeshaji la Umoja (Postal Operation Council-POC) kwa kushirikiana na Uswis wakati wa mikutano inayoendelea ya Baraza la Uendeshaji la Umoja huo
 
Aidha, kikao hicho cha Kamati namba 2 cha Baraza la Uendeshaji la Umoja wa Posta Duniani, kimeongozwa na Bw. Constantine Kasese ambaye ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Bishara wa Shirika la Posta Tanzania akishirikiana na Mwenyekiti mwenza Bw. Aime Theubet wa Posta ya Uswis wakati wa vikao vya Baraza hilo, jijini Berne ,Uswiss. 
 
Ujumbe wa Tanzania umewakilishwa na wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Shirika la Posta Tanzania. 
 
Tanzania ni mjumbe katika Baraza la Uendeshaji na lile la Utawala la Umoja wa Posta Duniani ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja huu Tanzania ilifanikiwa kuchaguliwa kuingia kwenye mabaraza yote mawili muhimu ya maamuzi katika Mkutano Mkuu uliofanyika jijini Abidjan,Ivory Coast Agost,2021. 
 
 
Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano, 
Shirika la Posta Tanzania. 
 
Picha zaidi za tukio hilo. 
 
 IMG 20220516 WA0004
 
 
 IMG 20220516 WA0017
 
 
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!