SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LATIKISA KWENYE WIKI YA WAMACHINGA DODOMA.

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LATIKISA KWENYE WIKI YA WAMACHINGA DODOMA.
IMG 20220517 WA0068
 
 
Shirika la Posta Tanzania limeshiriki mafunzo kwa Viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) yanayotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center, Jijini Dodoma.
 
Mafunzo hayo yaliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Bi. Zainab Chaula yaliyolenga kuwajengea uwezo Wajasiriamali wadogo na Machinga katika matumizi ya kidijiti, mifumo ya kiteknolojia, faida za Anwani za Makazi na Biashara Mtandao yameanza tarehe 16 Mei na  yanatarajiwa kumalizika 20 Mei 2022.
 
Aidha Shirika la Posta Posta limeshiriki mafunzo hayo kama mmoja wa Wadhamini wakuu na Mtoa mada wa mafunzo hayo, ambapo kupitia Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Amos Milinga na Meneja Biashara Mtandao wa Shirika la Posta Bw. Kulwa Fifi walitoa wasilisho la Shirika hilo na namna litakavyoshirikiana na Wamachinga katika kuendesha Biashara mtandao. 
 
Imetolewa na 
Ofisi ya Mawasiliano 
Shirika la Posta Tanzania.
 
 
IMG 20220517 WA0066
 
IMG 20220517 WA0063
 IMG 20220517 WA0065
 
 
 IMG 20220517 WA0064
 
IMG 20220517 WA0059
 
 
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!