RAIS SAMIA ATEMBELEA POSTA YA OMAN.

RAIS SAMIA ATEMBELEA  POSTA YA  OMAN.

IMG 20220615 WA0005

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametembelea Shirika la Posta Oman, tarehe 14 Juni,2022  kujionea utendaji wa Posta hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi nchini humo.

Aidha, ziara hiyo imekuja siku chache mara baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano wa kibiashara baina ya Shirika la Posta Tanzania na Shirika la Posta Oman kwenye maeneo mbalimbali ya kibiashara ili kuleta ufanisi na kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 31 Mei 2022, jijini Dar es salaam, Tanzania, Shirika la Posta Tanzania na Shirika la Posta Oman walitiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara kwenye maeneo 17 ikiwemo Biashara mtandao, huduma za usafirishaji pamoja na uchapaji Stempu za kihistoria ikizingatiwa nchi hizi mbili zina uhusiano wa kihistoria.


Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania
14.06.2022

 

IMG 20220615 WA0007

 

IMG 20220615 WA0001

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!