📍ARUSHA 📍

📍Arusha 📍

24A3558D D2BE 4543 A354 92F474B68C6C

 Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo(kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (kushoto), wakiwa katika jengo la Makao makuu ya Umoja wa Posta Afrika, Jijini Arusha.

 Na mwandishi wetu,Arusha

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Mbodo amekutana na kufanya mazungumzo na katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Ndg. Sifundo Chief Moyo kuhusu ushirikiano baina na Shirika la Posta Tanzania na Umoja huo kuwa Nchini, Tarehe 22 Julai, 2022 jijini Arusha, Tanzania.

Mazungumzo hayo yalifanyika Jijini Arusha katika ofisi za Makao Makuu ya Umoja huo yaliambatana na ziara fupi ya katika jengo jipya la Makao Makuu ya PAPU linaloendelea kujengwa jijini humo

Aidha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika pamoja na Postamasta Mkuu katika mazungumzo yao wametilia mkazo suala la mchango wa Posta kwenye kuchangia ujenzi wa uchumi na kuendelea kusisitiza matumizi ya Teknolojia katika utoaji wa huduma za Posta kwa biashara endelevu.

Imetolewa na; 
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.
27 Julai,2022.

Picha zaidi za tukio hilo:

1816201A 24A0 4554 B22D EA52F522936E

 078FA525 B4D4 492F BA38 A3687A6D2508

 

 

 

 

 

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!