HUDUMA YA MIZIGO MIKUBWA (POST CARGO) NDANI YA MBEYA.
HUDUMA YA MIZIGO MIKUBWA (POST CARGO) NDANI YA MBEYA.
Na mwandishi wetu,mbeya
Posta tupo katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) katika viwanja vya John Mwakangale, Uyole, Mkoani Mbeya kukupatia huduma ya kusafirisha mizigo mikubwa yaani (Post Cargo).
Maonesho hayo yenye kauli mbiu isemayo, "Kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi" yanayoanza tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2022 yanahusisha Taasisi mbalimbali na wadau wa Kilimo na Ufugaji Nchini ambapo Posta kama mmoja wa wadau hao, inashiriki Maonesho hayo kama mdau muhimu wa sekta ya usafirishaji wa mazao pamoja na bidhaa zake kupitia huduma ya Usafirishaji wa Mizigo Mikubwa ' Posta Cargo' na huduma ya uuzaji wa mazao kupitia duka lake la Mtandao "Posta Online Shop".
Tunawakaribisha wadau mbalimbali kutembelea banda la Shirika la Posta katika maonesho hayo ili kujipatia huduma zetu kwa haraka na ufanisi.
Imetolewa na
Ofisi ya Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania.
Picha zaidi,