VIONGOZI WA POSTA WATAKIWA KUWA WABUNIFU

VIONGOZI WA POSTA WATAKIWA KUWA WABUNIFU

B98FA6FF 037E 4475 A155 D077BD63DE6C 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo akizungumza wakati akifunga rasmi Kikao Kazi cha viongozi wa Shirika hilo, katika ukumbi wa mikutano wa Baraza Chuo Kikuu SUA, mjini Morogoro 

 

Na mwandishi wetu, Morogoro
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania, Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo amewataka Viongozi wa Shirika la Posta nchini kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Ameyasema hayo tarehe 05 Agosti, 2022 wakati alipokuwa akifunga rasmi Kikao Kazi cha Viongozi hao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza wa Chuo Kikuu SUA, mjini Mororgoro.

Akizungumza wakati akifunga kikao hicho Brigedia Generali Mstaafu Mabongo amewataka Viongozi hao kuwajibika kila mmoja katika nafasi yake huku akitoa wito kwa Viongozi hao kubadilisha mitazamo yao Ili kufanya kazi kwa Ubunifu wakati wa kutimiza majukumu yao ili kuendelea kutoa huduma zinazoendana na mahitaji ya wananchi.

Aidha, Mwenyekiti Mabongo amesisitiza kikao hicho kiwe chachu ya kuhakikisha kila kiongozi anatoka na mabadiliko yatakayoongeza ufanisi katika eneo lake la kazi, kubuni mbinu mpya za kiutendaji pamoja na kufanya tathmini ya utendaji wao ili kuongeza tija kwa Shirika.

“Niwatake nyote baada ya kutoka hapa, mkakae na kufanya tathmini na wafanyakazi wenu kila mmoja kwenye eneo lake hii itasaidia kuchukua hatua stahiki za maboresho ili matarajio ya Serikali yaweze kufikiwa”. Amesema Mwenyekiti Mabongo.

Sambamba na hilo Brigedia Generali Mstaafu Mabongo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Postamasta Mkuu pamoja na Menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania kwa juhudi mbalimbali zinazoendelea kufanywa katika mageuzi ya Shirika yenye lengo la kuboresha huduma zinazotolewa ili ziwafikie wananchi wengi zaidi na zikidhi mahitaji yao halisi.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Mabongo, amekabidhi zawadi kwa mikoa mitatu iliyofanya vizuri katika utendaji, mikoa hiyo ni Lindi (1), Morogoro (2) na Mara (3) mikoa hii iliweza kutimiza vigezo vyote vitatu vya upimo.

Vilevile alikabidhi zawadi kwa kiongozi hodari kwa upande wa Mameneja mikoa (Joyce Chirangi-Mara) na Eric Maximillian (Makao Makuu).

Kwa upande wake Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo, amemshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo kwa kufika na kufunga kikao kazi hicho na kuahidi kuwa, watazingatia maelekezo yote kwa niaba ya Menejimenti yake pamoja na wafanyakazi kwa maslahi mapana ya Shirika na umma wa watanzania kwa ujumla.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania;
05 Agosti, 2022

Picha zaidi za tukio hilo,

 D5CA9E40 79F9 483D AD6C 4A36EA088687

 Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo akizungumza wakati wa Kikao Kazi cha viongozi wa Shirika hilo, kilichofungwa rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Brig. Jen. Mstaafu Yohana Mabongo (hayupo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa Baraza Chuo Kikuu SUA, mjini Morogoro 

1659C699 D74F 48FA BE7E A11A645A1017

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo akikabidhi zawadi kwa Meneja wa Posta Mkoa wa Lindi, Riziki Ruhongole kwa mkoa huo kuwa wa kwanza katika utendaji kwa mwaka 2021/2022 mara baada ya kufunga rasmi Kikao Kazi cha viongozi hao, katika ukumbi wa mikutano wa Baraza Chuo Kikuu SUA, mjini Morogoro

 

56EF382E 45CB 456E AB3E 80B2AB40DA12

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo akikabidhi zawadi kwa Meneja wa Posta Mkoa wa Morogoro, Magreth Mlyomi kwa mkoa huo kuwa wa pili katika utendaji kwa mwaka 2021/2022 mara baada ya kufunga rasmi Kikao Kazi cha viongozi hao, katika ukumbi wa mikutano wa Baraza Chuo Kikuu SUA, mjini Morogoro

 

F51BC188 4CD3 44E9 94C4 DD47C7BAD750

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo akikabidhi zawadi kwa Katibu wa Shirika hilo Erick Maximilliam kwa kuwa Kiongozi hodari kwa Makao Makuu katika utendaji kwa mwaka 2021/2022 mara baada ya kufunga rasmi Kikao Kazi cha viongozi hao, katika ukumbi wa mikutano wa Baraza Chuo Kikuu SUA, mjini Morogoro

 5D12FEE2 100B 4147 9BBE 0171865669F2

 Meneja wa Shirika la Posta mkoa wa Morogoro Magreth Mlyomi akitoa neno la shukrani mara baada ya kufungwa rasmi kwa Kikao Kazi cha viongozi wa Shirika hilo, katika ukumbi wa mikutano wa Baraza Chuo Kikuu SUA, mjini Morogoro

 

2CEDB1DF 9BCE 417C 8933 BDE4BD5D6265

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo akiwa katika picha za pamoja na viongozi wa Shirika hilo mara baada ya kufunga rasmi Kikao Kazi cha viongozi hao, katika ukumbi wa mikutano wa Baraza Chuo Kikuu SUA, mjini Morogoro

 

 F334115C AA8D 41DE B60E 5B9B02B0E722

 

 

 

 

 

 

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!