WAKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA NA MLELE WAFURAHIA HUDUMA ZA SHIRIKA LA POSTA.
WAKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA NA MLELE WAFURAHIA HUDUMA ZA SHIRIKA LA POSTA.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Mhe. Filberto Sanga(kushoto mwenye shati nyekundu) na Mkuu wa Wilaya wa Tanganyika Mhe. Onesmo Buswelu(kulia) wakisikiliza maelezo ya huduma za Posta kutoka kwa Meneja Msadizi wa Posta Mkoa wa Mbeya, Ndg. Peter Songela(hayupo pichani).
Na mwandishi wetu,Mbeya
Leo tarehe 6 Agosti 2022, Shirika la Posta Tanzania limepata nafasi ya kutembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Onesmo Buswelu na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Mhe. Filberto Sanga ambao kwa pamoja wamelipongeza Shirika la Posta kwa uboreshaji wa huduma zake ikiwemo huduma ya usafirishaji wa mizigo mikubwa ' Post Cargo' pamoja na huduma ya EMS.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara yao katika Banda Shirika la Posta Tanzania liliko kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale, Uyole, Mkoani Mbeya.
Aidha, Viongozi hao walitoa wito kwa Shirika la Posta kuongeza ufanisi wa huduma zake za usafirishaji hasa katika Mkoa wa Katavi ambapo huduma ya Usafirishaji wa Mizigo mikubwa "Post Cargo" inahitajika sana ili kuwezesha usambazaji wa Mazao ya wakulima Mkoani humo.
Shirika la Posta Tanzania linashiriki maonesho hayo kama mtoa huduma za Usafirishaji na Biashara mtandao ambapo wateja wamekuwa wakipata maelezo na huduma mbalimbali za Shirika kupitia banda la Posta.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania.
Picha zaidi za tukio hilo,
Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Mhe. Filberto Sanga(wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe. Onesmo Buswelu(wa pili kushoto) wakisikiliza maelezo ya huduma za Shirika la Posta kutoka kwa Meneja Msadizi wa Posta Mkoa wa Mbeya, Ndg. Peter Songela(kulia).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Mkoani Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Onesmo Busweluwa(kushoto aliyekaa) na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Mhe. Filberto Sanga(kulia aliyekaa) walipotembelea banda la Shirika hilo wakati wa maonesho ya Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale, Uyole, Mbeya.