📍Zanzibar📍

📍Zanzibar📍

0C5DE71A 64D8 4248 878F 4B26DEAB8089

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akipata maelezo ya anwani ya Makazi ya nyumbani kwake kutoka kwa Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, SMZ Mhe. Dk. Khalid Salum Mohamed (kushoto) mara baada ya kuwekwa nyumbani kwake Migombani, Zanzibar

 

Na mwandishi wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito Kwa Wananchi wote wa Unguja na Pemba kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi inakayofanyika tarehe 23 Agosti, 2022.

Aliyasema hayo tarehe 22 Agosti, 2022 wakati akipokea Anwani ya Makazi ya Nyumbani kwake Migombani iliyoratibiwa na Shirika la Posta Tanzania kwa ushirikiano na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Anwani hiyo ya Makazi imekabidhiwa kwake na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, SMZ Mhe. Dk. Khalid Salum Mohamed aliyeambatana na Meneja Mkaazi wa Posta Zanzibar Bwana Ahmad Rashid na Meneja wa Posta Dar es salaam Bwana Arubee Ngaruka waliomwakilisha Postamasta Mkuu Bwana Macrice Mbodo.

Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania.
22 Agosti, 2022.

picha zaidi za tukio hilo,

A90AC701 3945 4FA5 A846 F368E388A1AE

 806F6622 0994 47B6 979E 05A7C85505D0

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Wizara Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, SMZ pamoja na Shirika la Posta Tanzania, mara baada ya kuwekwa Anwani ya Makazi ya nyumbani kwake Migombani, Zanzibar

 7E8C6089 71F8 42AB A6B6 7AD10471FBB5

9EF20FB6 E78D 4858 B8B8 0CA534C42FC7

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!