NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI ATEMBELEA OFISI ZA POSTA - ZANZIBAR

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI ATEMBELEA OFISI ZA POSTA - ZANZIBAR

79F8CCF8 C794 4851 BB64 A4542238A23E

 Afisa wa Shirika la Posta Zanzibar Bw. Khamis Ame Mohammed (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla kuhusu huduma mbalimbali za Shirika zinazotolewa katika Ofisi za Posta mjini Zanzibar

 

 

Na mwandishi wetu, Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla kwa mara ya kwanza tarehe 30 Agosti, 2022, amefanya ziara yake katika Ofisi Kuu za Shirika la Posta Tanzania, mjini Zanzibar.

Lengo la ziara yake ni kujionea namna Shirika la Posta linavyofanya shughuli zake katika kuwahudumia wananchi hususani katika eneo la usafirishaji wa barua, nyaraka, mizigo na vipeto, mjini humo.

Aidha, Bw. Mohammed Abdulla ametumia nafasi hiyo kulitaka Shirika la Posta Tanzania kuendelea kuboresha mifumo yake ili kurahisisha utendaji kazi utakaowezesha kuendelea kutoa huduma zenye ubora kwa wananchi

Sambamba na hilo, Naibu Katibu Mkuu amelipongeza Shirika la Posta kwa jitihada zake mbalimbali za kuendelea kuboresha huduma zake ili kuendana na maendeleo ya Teknolojia Pamoja na mahitaji ya wananchi.

Ziara ya Naibu Katibu Mkuu ilienda sambamba na ukaguzi wa minara 42 itokanayo na mradi wa "Rural Telecommunication Border & Special Zone Phase 7 (BSZPH7)" iliyojengwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na kampuni ya  Tigo-Zantel.

Ukaguzi huo ulifanywa na Naibu Katibu Bw. Mohamed Khamis Abdulla na Posta imeshiriki kama mdau wa Mawasiliano nchini aliyeshiriki ziara hiyo ni Meneja Mkaazi (TPC) Zanzibar Bw. Ahmad Mohammed Rashid.

 

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania,
30 Agosti, 2022.

 Picha zaidi za tukio hilo

308DD953 A57D 4FE9 841B 2B45387A0548

 

3A4584BA FB66 4760 AFB7 62E8C8CC5A9C

 6D5D350C 410F 4082 9A49 2BEF0792CF3A

 Picha na Matukio mbalimbali wakati Meneja Mkaazi (TPC) Zanzibar Bw. Ahmad Mohammed Rashid aliposhiriki ziara ya ukaguzi wa minara 42 ya Mawasiliano itokanayo na mradi wa Rural Telecommunication Border & Special Zone Phase 7 (BSZPH7) iliyifanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla mjini Zanzibar

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!