MAONESHO YA KIMATAIFA YA BISHARA MARA

MAONESHO YA KIMATAIFA YA BISHARA MARA 

5DED0011 B98F 45C0 975D 31699F6D5EB6

 Mratibu wa shughuli za mikoa kutoka Posta Makao Ndg Khamis Swedi wa pili kushoto, akitoa ufafanuzi kuhusiana na biashara zinazotolewa na Shirika la Posta Tanzania kwa baadhi ya wateja waliotembelea banda la Posta lililopo katika maonesho ya kibiashara yanayoendelea katika viwanja vya Mukendo, mjini Musoma, Mkoani Mara.

Na mwandishi wetu, Mara
Wananchi wamiminika kwenye Banda la Posta mjini Musoma 

Wananchi mbalimbali wamemiminika kwenye Banda la Shirika la Posta Tanzania lililopo kwenye viwanja vya Mukenda mjini Musoma ambako maonesho ya kimataifa ya kibiashara yanafanyika.

Ndani ya Banda hilo, wananchi wamepata nafasi ya kujionea mageuzi mbalimbali katika utoaji wa huduma za Posta ikiwemo Duka Mtandao, Sanduku la Kielectroniki la Posta, Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni, Biashara za Uwakala wa Bima, Mabenki na ukataji wa tiketi za ndege za ATCLna nyinginezo.

Wananchi wamepata nafasi ya kujifunza huduma mpya zinazotolewazo na Shirika na wengi wao wamejisajili na huduma za Duka Mtandao na Sanduku la Kielectroniki zikiwa ni huduma za kuwarahisishia kufanya shughuli zao ikiwemo biashara ndogondogo na mawasiliano na ufikishaji wa bidhaa zao pale wanapohitaji kwa wakati kwa gharama nafuu na usalama.

Meneja wa Posta Mkoa wa Mara Bi Joyce Chirangi, amewaomba wananchi wote kujisajili na kutumia huduma za Shirika kwa kuwa ni nafuu na za hakika.

Aidha, Meneja huyo amewasisitiza kuwa Shirika limejipanga vizuri Ili kuhakikisha linawafikia watanzania na wateja wote popote walipo na kuwapatia huduma bora.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano

Shirika la Posta Tanzania.

09 Septemba, 2022.

Picha zaidi za tukio hilo,

7EB7A642 18A4 4578 B0C0 320EC60F2418 

 6CAF2D68 CFF0 48E4 AEF8 94F6D6BCE4A9

 Meneja wa Posta Mkoa wa Mara Bi, Joyce Chilangi wa pili kutoka kushoto akiwa na baadhi ya wafanyakazi wanaoshiriki maonesho ya Mara Business Expo 2022.

 5F0A2472 9463 4B10 91D3 DC78D634E3CB

 

A60F3871 355C 4994 BE36 0F27AA6E5E8C 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!