POSTA YASHIRIKI KONGAMANO LA AfCFTA

POSTA YASHIRIKI KONGAMANO LA AfCFTA

 8CE55B38 1735 4FC7 A805 C1095227C69D

 Na mwandishi wetu, Dar es salaam


-Huduma mbalimbali za Posta zinatolewa katika kongamano hilo

Shirika la Posta Tanzania linashiriki kwenye Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Ufunguzi rasmi wa Kongamano hilo umefanywa leo tarehe 12 Septemba, 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

 

Kongamano hilo ni la siku tatu na lina lengo la kuwawezesha wanawake na vijana kufanya biashara zao kwa uhuru huku wakinufaika na soko lililopo.

Aidha, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo amehudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo lililoambatana na maonesho ya biashara na huduma mbalimbali limehudhuriwa na viongozi kutoka ndani na nje ya nchi, huku Posta ikishiriki kama mdau wa biashara nchini na Afrika kwa ujumla.

Shirika la Posta lipo ukumbini hapo kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma huduma za Sanduku la kieletroniki (kupitia Posta Kiganjani), Duka Mtandao la Posta pamoja na huduma ya kutuma mizigo, barua,vipeto na vifurushi.

Katika ufunguzi huo, Bw. Macrice Mbodo aliambatana na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika Bw. Constantine Kasese.

 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano,
*Shirika la Posta Tanzania,*

kieletroniki (kupitia Posta Kiganjani), Duka Mtandao la Posta pamoja na huduma ya kutuma mizigo, barua,vipeto na vifurushi.

Katika ufunguzi huo, Bw. Macrice Mbodo aliambatana na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika Bw. Constantine Kasese.

 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania,
12 Septemba ,2022

picha zaidi za tukio hilo,

F504AD5B 14B6 41AD B4DA 23C6B90D40F1

 Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo (kushoto) akiambatana na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika Bw. Constantine Kasese (kulia) wakati wakiwasili katika Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

 CDAAD67B B65C 44CE B7EA 3C73186A7FE3

 Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akisalimiana na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo mara baada ya Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

  BA9A8459 2ED5 48B1 9AC2 CCA24166A808

 Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Amour Hamil Bakari (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo mara baada ya Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

21E27BF2 CC95 4DBA BA4A 695742916688 

 Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Posta wanaotoa huduma katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Aliyeketi kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika Bw. Constantine Kasese.

 

 

 

 

 

 

 

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!