MHANDISI KUNDO: BORESHENI HUDUMA ZA POSTA ILI ZIANDANE NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA YALIYOKO DUNIANI KWA SASA.

MHANDISI KUNDO: BORESHENI HUDUMA ZA POSTA ILI ZIANDANE NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA YALIYOKO DUNIANI KWA SASA.

 

C29879C2 09E1 4942 9DE2 13210C471D78

 Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) akizungumza wakati alipokuwa akifungua Jukwaa la kwanza la watoa huduma wa Sekta ya Posta na Usafirishaji, kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Nnauye (Mb) lilioandaliwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO), katika hoteli ya Mount Meru, Arusha tarehe 2 Novemba 2022.

 

Na mwandishi wetu, Arusha

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) ameyataka Mashirika ya Posta ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuchangamkia fursa za mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea duniani kwa sasa ili sekta hiyo iweze kutoa huduma bora zinazokidhi matakwa ya wateja.

Mhandisi kundo ameyasema hayo leo tarehe 2 Novemba 2022 katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha, wakati akifungua Jukwaa la kwanza la watoa huduma wa Sekta ya Posta na Usafirishaji, lilioandaliwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO), huku likihusisha Mashirika yote ya Posta kutoka nchi za Afrika mashariki.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnaye(Mb), Mhandisi Kundo ameeleza kuwa jukwaa hilo lenye lengo la kuwakutanisha pamoja wadau wa sekta ya posta na kubadilishana uzoefu, waangalie namna bora zaidi ya kuboresha huduma za posta Kwa kuondoa changamoto ndogo ndogo zinazoikumba sekta ya Posta hasa baada ya utandawazi na teknolojia mpya na kujikita kwenye Biashara mtandao na huduma za fedha huduma jumuishi za kifedha Kwa kufanya mabadiliko mahsusi ya kidijitali.

Mhandisi Kundo aliongeza kuwa, jukwaa hilo ni la kwanza kwa Mashirika ya Posta ya Jumuiya hiyo liwe chachu ya kutoa huduma huduma za posta zilizoboreshwa na kuwafikia wananchi wengi kwa haraka, ufanisi na kwa gharama nafuu kupitia teknolojia za kisasa.

"Napenda kumshukuru Rais  Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri na rafiki sana ya kidiplomasia yanayotoa nafasi Kwa taasisi hizi kukutana Kwa uhuru na kujadiliana namna ya kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili watoa huduma mbalimbali katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hii inatokana na namna ambavyo Mh Rais Samia amekuwa kinara wa kuhakikisha mifumo na miundombinu ya mawasiliano nchini inazidi kurahisishwa na kuboreshwa kwa ajili ya maslahi ya wananchi" alisema Mhandisi Kundo.

Vilevile, mhe. Kundo alitumia nafasi hiyo kulipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa mabadiliko mengi ya kidijitali ambayo Shirika hilo inayafanya kwa sasa katika huduma zake ikiwemo uwepo wa Posta kiganjani ambayo ni mpya inayounganisha hduma zote za Posta Tanzania kigajanja kwa mteja. Hivyo anajivunia sana kwa Tanzania kupata fursa ya kuandaa jukwaa hilo la kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Naye Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya  Mawasiliano ya Afrika Mashariki, Dkt. Alli Yahaya Simba amesema kuwa lengo la jukwaa hilo ni kuinua na kuipa mwelekeo sekta ya Posta ya Afrika Mashariki, kwani kuna fursa nyingi sana kwenye sekta ya usafirishaji, mabadiliko ya kidijitali pamoja na biashara mtandao.

Dkt. Simba amesema kuwa, kupitia Jukwaa hilo wadau wa Sekta ya Posta watapata nafasi ya kuzungumzia namna Sekta ya Posta itakavyosaidia wananchi wake kiuchumi hasa kwa kuzingatia kuwa huduma za kifedha na biashara mtandao ni moja ya majukumu ya Masharika ya Posta.

Aliongeza kuwa, EACO iko katika mchakato wa kuifanya iwe Taasisi Kitovu cha TEHAMA kwa Nchi za Afrika Mashariki ili kuhakikisha yale matunda  yanayotokana na Sekta ya Posta yanaonekana na kuwafikia wananchi wa Jumuiya hiyo kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo amesema kuwa, ni heshima kubwa kwa Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na EACO kuandaa Jukwaa hilo la kwanza kwa Posta za Afrika Mashariki ambalo  halikuwahi kufanyika hapo kabla.

"Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kupitia mamlaka zake kwa kuturuhusu sisi kuandaa na kufanya mkutano huu. Mageuzi ya posta yetu ya Tanzania yanayoendelea kufanyika kwa sasa yamekuwa kivutio kwa Posta zingine za Afrika Mashariki na  kupitia mkutano huu tutatumia fursa hii kuonyesha namna ambavyo tunatoa huduma zetu kidigitali ili na wenzetu waweze kupata uzoefu kupitia kwetu" Amesema Postamasta Mkuu Mbodo.

Aidha ameeleza kuwa, wameona umuhimu wa kukaa pamoja kama Wakuu wa Posta wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kutafakari namna ambavyo Taasisi hizo zitaweza kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kushiriki katika mchango wa maendeleo ya Jumuiya ya Afrika  Mashariki. 

Naye, Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika, Ndugu Sifundo Chief Moyo ameyapongeza Mashirika ya Posta ya Afrika mashariki kwa kuamua kukaa pamoja na kubadilishana uzoefu na mbinu mpya za kuendesha mashirika hayo kwa ufanisi na faida.

Jukwaa hilo la siku tatu, lililoanza leo linahusisha wadau wa Sekta ya Posta na Usafirishaji kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Wakuu wa Taasisi za Posta kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, South Sudan pamoja na Wawakilishi kutoka Umoja wa Posta Duniani na Umoja wa Posta Afrika.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania. 

Picha zaidi za tukio hilo,

F559BA63 115F 4D91 964F 4C9C3274AC6D

Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Ndugu Sifundo Chief Moyo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la kwanza la watoa huduma wa Sekta ya Posta na Usafirishaji, lilioandaliwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO).

AD06ABD3 E5EE 4B55 82CF F9D2D0324415

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la kwanza la watoa huduma wa Sekta ya Posta na Usafirishaji, lilioandaliwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO), katika hoteli ya Mount Meru, Arusha tarehe 2 Novemba 2022.

53373008 4426 4CFF A52B FCA182BFA0DF

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Ndugu Mohammed Abdulla, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la kwanza la watoa huduma wa Sekta ya Posta na Usafirishaji, lilioandaliwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO), katika hoteli ya Mount Meru, Arusha tarehe 2 Novemba 2022.

340674EB 76A3 4BBD 8E61 73C086247450

1DA9F426 EF3C 408F B9A4 674676D8086A 

D0514F7C 0C09 4B7B A2E0 835408DA4C6B 

 Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb)(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Afrika Mashariki, Dkt. Ally Simba (Kushoto) wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la kwanza la watoa huduma wa Sekta ya Posta na Usafirishaji, lilioandaliwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO), katika hoteli ya Mount Meru, Arusha tarehe 2 Novemba 2022.

 D927C87A 7D7B 49E8 AA2E 087E473CC63F

 064214C5 DE6E 4D0A 9F00 02047592D56A

 D36DE25F 010B 4446 AC69 2D6990880A3F

 A9406F00 52AF 4D77 95BD F9588F96AA6C

 949BB28D 08CE 4907 B054 7D89E2AC1CC7

 DE745E11 CF7E 4FBF B1E4 541E81E3E6E7

48617D5A 1873 4997 9C67 DCFA4AEC2BAF 

 

 

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!