📌 POSTA ZA AFRIKA MASHARIKI, ZAJIDHATITI KUTOA HUDUMA ZAO KIDIJITALI.

📌 POSTA ZA AFRIKA MASHARIKI, ZAJIDHATITI KUTOA HUDUMA ZAO KIDIJITALI.
 624AD1D8 3E26 474E AA48 AE8FA15E2A39

 

 

Na mwandishi wetu, Arusha
Tarehe 3 Novemba 2022 Wadau wa huduma za Posta na Usafirishaji kutoka nchi za Afrika Mashariki wamekutana tena na kujadiliana namna Mashirika ya Posta ya ukanda wa Afrika Mashariki yanavyoweza kushirikiana na Mamlaka za Mawasiliano pamoja na watunga Sera kutoka nchi zao katika kukabiliana na mabadiliko ya kidijiti katika sekta ya usafirishaji, biashara mtandao na huduma za kifedha.
 
Majadiliano hayo yamefanyika katika hoteli ya Mount Meru Arusha ambapo watoa mada kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA) walitoa mawasilisho ya namna ambavyo Taasisi hizo zinavyosaidia kudhibiti mawasiliano na ukuaji wa sekta ya Posta na usafirishaji ndani ya nchi zao.
 
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Emmanuel Manasseh alitoa wasilisho lililoeleza namna ambavyo Mamlaka hiyo inadhibiti uhalifu wa mitandao pamoja na kufuatilia kwa karibu utoaji wa taarifa mitandaoni, usalama wa matumizi ya fedha mtandao, pamoja na Biashara mtandao zinazofanywa na watu binafsi na Taasisi likiwemo Shirika la Posta Tanzania.
 
Aidha, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA), Ndugu Bernard Nderitu alieleza namna Mamlaka hiyo inavyoshirikiana na Shirika la Posta Kenya katika kuleta mabadiliko chanya ya teknolojia ya mawasiliano, biashara mtandao na huduma jumuishi za kifedha.  
 
Kwa upande wa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Burundi Bi. Le’a Ngabire alizungumzia namna Shirika hilo lilivyopiga hatua katika matumizi ya mitandao katika huduma za kifedha, ambapo watumiaji wa huduma za Posta Burundi wanavyoweza kulipia huduma za Shirika hilo kupitia simu za mkononi, na kwamba Shirika hilo linaelekea katika kuanzisha biashara mtandao kwani ndio mwelekeo wa dunia kwa sasa.
 
 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Posta Rwanda, Ndugu Celestine Kayitare alizungumzia namna Shirika hilo lilivyoandaa mradi wa mabadiliko ya kidijitali uitwao ‘Kuwezesha kesho yako' (Enabling the future project), huku wakitarajia kuanzisha maghala na vituo vya biashara mtandao kutokana na kuwa na mifumo mizuri ya Anwani za wateja. Tayari Rwanda wanalo jukwaa la Biashara Mtandao lijulikanalo kama ‘Rwanda Mart’ na hadi sasa wamesajili Wajasiliamali na Wafanyabiashara 460.
 
Jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji limeendelea leo na kikao chake kwa siku ya pili huku likihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika, Ndugu Sifundo Chief Moyo, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo na Wakuu wa Mashirika ya Posta pamoja na wawakilishi kutoka Posta za Afrika Mashariki, Umoja wa Posta Afrika na Umoja wa Posta Duniani.
 
Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania,
3 Novemba 2022.

Picha zaidi za tukio hilo,

FF2BAD84 80C9 4AA6 AC6A 7207941E50C5

 Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo, akisikiliza jambo wakati wa kikao cha pili wa jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania(TPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO), tarehe 3 Novemba 2022 kwenye hoteli ya Mount Meru, Arusha.

 B3DA8DA1 DEE1 4E4F A109 F557668F316B

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika(PAPU), Ndugu Sifundo Chief Moyo, akisikiliza jambo wakati wa kikao cha pili cha Jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki (EACO), tarehe 3 Novemba 2022 jijini Arusha.

6581028E 77FC 4BE8 B0DD EDEC4BD1D26F 

 Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya  Mawasiliano ya Afrika Mashariki,(EACO) Dkt. Ally Simba akiuliza swali, wakati wa kikao cha pili cha Jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki (EACO), tarehe 3 Novemba 2022 jijini Arusha.

 80C123C9 952A 46E5 A11A E90033459F85

 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Emmanuel Manasseh akiwasilisha wasilisho wakati wa kikao cha pili cha Jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki (EACO).

 E40CD022 1082 49B2 B6E2 FFF4DA5343AD

 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA), Ndugu Bernard Nderitu akiwasilisha wasilisho wakati wa kikao cha pili cha Jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki (EACO), tarehe 3 Novemba 2022 jijini Arusha.

 AD6154EA 8CE3 4BD8 9011 B5AC51399692

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta Rwanda, Ndugu Celestine Kayitare, akiwasilisha wasilisho wakati wa kikao cha pili cha Jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki (EACO), tarehe 3 Novemba 2022 jijini Arusha.

 5B67D14A 57C0 404A 9290 E4D873D349A6

 Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Burundi Bi. Le’a Ngabire akiwasilisha wasilisho wakati wa kikao cha pili cha Jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki (EACO), tarehe 3 Novemba 2022 jijini Arusha.

 4CB5BA84 04D1 42A8 99A4 177E0CF28E1C

Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Constantine Kasese (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Posta Mkoa wa Arusha, Ndugu Athumani Msilikale (Kulia) mbele ya banda la Shirika hilo lililoko ndani ya ukumbi wa hoteli ya mount Meru Arusha, linakofanyika Jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki (EACO), tarehe 3 Novemba 2022 jijini Arusha. 

 B0E76099 F57A 4153 9986 746CA4C3C459

 7D13D86B E149 4A50 879F A1C45944C7C3

 1C6ED44C DED2 4274 BD80 3D1AA73F29FA

 A83FA9A4 3D49 4587 AE8A CC0DA5F077E9

7E3C4DB7 0DFC 4163 8F76 1B77EE98E577 

FB319ABB A24B 4425 8E68 F1047B7DF365 

 BECFD445 A2B2 4BEA A13B A1404C8401AB

C67E12D1 3949 4253 BC10 D18825495207 

CF841392 4097 4CAE 9020 895A96EE2237 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!