📌 JUKWAA LA KWANZA LA POSTA NA BIASHARA MTANDAO AFRIKA MASHARIKI.

📌 JUKWAA LA KWANZA LA POSTA NA BIASHARA MTANDAO AFRIKA MASHARIKI.

7F629120 F963 4548 A49F 63B4368C181F

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo, akiwasilisha wasilisho la Shirika hilo wakati wa kikao cha tatu cha jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania(TPC) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO), leo tarehe 4 Novemba 2022 kwenye hoteli ya Mount Meru, Arusha.

🔻Postamasta Mkuu aeleza Mafanikio ya Shirika la Posta katika kutoa huduma kidijitali.

 

Na mwandishi wetu, Arusha

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo ametoa wasilisho mbele ya Wakuu wa Taasisi za Posta za Afrika Mashariki wakati wa kikao cha tatu cha Jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki (EACO).

Wasilisho hilo limetolewa leo tarehe 4 Novemba 2022, katika hoteli ya Mount Meru, Arusha ambapo Postamasta Mkuu alieleza namna Posta ilivyopiga hatua ya kutoa huduma kidijitali ikiwemo kuanzisha APP ya Posta Kiganjani ambayo huduma zote za Shirika zitapatikana kiganjani kwa mteja kupitia simu yake ya mkononi au kompyuta Mpakato.

Postamasta Mkuu alieleza namna ambavyo Shirika limepata mafanikio makubwa katika eneo la usafirishaji ikiwemo kumiliki magari makubwa ya hadi tani 30 ambayo yanasafirisha bidhaa mbalimbali ndani na nje ya Nchi ikiwemo Uganda.

Aidha, Postamasta Mkuu alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuliwezesha Shirika la Posta kukua kiteknolojia na kuweka mazingira rafiki ya kidijitali ndani ya Nchi.

Jukwaa hilo la kwanza la Posta na Usafirishaji, limeshirikisha wakuu wa Taasisi za Posta za Nchi Afrika Mashariki, Viongozi wakuu wa Posta Afrika pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Umoja wa Posta Duniani,Bwana Mutia Muthusi.
Jukwaa hilo linatarajiwa kuhitimishwa leo tarehe 4 Novemba 2022.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania,
Tarehe 4 Novemba, 2022.

picha zaidi za tukio hilo,

223E5A1B 221F 4F9F B7AE 2A7503B5FDE4

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Kenya Ndugu Dan Kagwe, akiwasilisha wasilisho la Shirika la Posta Kenya wakati wa kikao cha tatu cha jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, lililoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania(TPC) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO), leo tarehe 4 Novemba 2022 kwenye hoteli ya Mount Meru, Arusha.

D5FDA26B FEF4 4E6E 9B17 348B6CBD23E5 

 Washiriki mbalimbali wa jukwaa la kwanza la Posta na Usafirishaji, wakimsikiliza Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo wakati akitoa wasilisho lake.

 C81F423B E53B 4043 A1DE 526FC784C957

 A1D91133 EB3A 4AB1 A689 5B64813414AB

88C2E1B8 9E28 4D04 B357 75A55C8D8113 

 6A2AF4EF DD25 4142 A9AC 4F05E6224DBB

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!