♦️UMOJA WA POSTA DUNIANI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA TANZANIA♦️

♦️UMOJA WA POSTA DUNIANI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA TANZANIA♦️

DC5EEDAB 9FB4 4FF6 B344 782E69AF55C8

 Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Umoja wa Posta Duniani Bw. Mutua Muthusi (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Shirika la Posta Tanzania wakati wa ziara yake katika Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.

Katikati ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Bw. Aron Oyye akimwakilisha Postamasta Mkuu wa Shirika hilo.

 

 

Na mwandishi Wetu, Dar es salaam

Azitaka Taasisi za Posta
kutumia fursa za
maendeleo ya kidijiti

Yaahidi kuweka mikakati
madhubiti ya kuwezesha
matumizi TEHAMA kwenye
sekta ya Posta duniani

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Umoja wa Posta Duniani Bw. Mutua Muthusi, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Umoja huo Bw. Masahiko Metoki ameahidi kuendelea kuwezesha Sekta ya Posta katika kusambaza huduma zake kimataifa

Ameyasema hayo tarehe 05 Novemba, 2022, wakati alipofanya ziara yake Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam

Lengo la ziara hii ni kutembelea na kukagua ofisi ya Mtaalamu wa Miradi wa Umoja wa Posta Duniani kwa Ukanda wa Afrika Mashariki zilizopo katika Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania,jijini Dar es Salaam

Katika ziara yake Bw. Muthusi, ameeleza kuwa Mashirika ya Posta Duniani yanapaswa kutumia fursa ya maendeleo ya kidigitali katika kuboresha huduma zake ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Aidha, ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais wake Mhe. @samia_suluhu_hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kidigitali katika Tanzania huku ikilirahishia Shirika la Posta Tanzania kutoa huduma zake sambamba na mahitaji ya wananchi

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Maendeleo Bw. Mutua Muthusi, ametembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Bakari Jabiri, katika mazungumzo yao ameipongeza Mamlaka hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuwezesha Mawasiliano nchini hususani katika Sekta ya Posta

Itakumbukwa kuwa,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Posta Tanzania imepewa heshima na Umoja wa Posta Duniani ya kuanzisha Ofisi za Umoja huo kwa Ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na kutoa Mtaalamu wa Kuratibu Miradi kwa Ukanda huo (UPU Field Project Expert for East Africa Sub-Region).

Picha zaidi za tukio hilo,

 B7BF894C 0AEF 40FC 9DB0 82636731EA33

 592BD644 FA62 4D66 9CC9 6FDA712CB0E4

 Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Bw. Aron Oyye kwa niaba ya Postamasta Mkuu wa Shirika hilo akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Maendeleo wa UPU Bw. Mutua Muthusi (kushoto) mara baada ya ziara yake katika Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.

 753DBE1C D58F 4D61 8AEC 2D503FB7104E

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Maendeleo wa UPU Bw. Mutua Muthusi (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mamlaka wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Viongozi wa Shirika la Posta Tanzania mara baada ya ziara yake katika Makao Makuu ya TCRA, jijini Dar es Salaam.

Katikati ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Bakari Jabiri

 D3275B20 8717 453F AF5D 1D549BDE0237

 4504FBA8 1D60 4EEE A85F 74C345EBD681

 612DBA3C 0AB6 44F0 9CB2 B270802946C9

 552E5020 8456 453B 80F3 3C3A1B0A5764

 40191085 581C 4B43 A593 B99A22065C2E

 A89A3FB8 44CA 410B 91B1 1371993EB1CC

E9286378 388B 420B B995 5769E3AF220B 

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!