♦️ MBODO : “KIKAO CHENU KIJIKITE KUJADILI MWELEKEO WA POSTA KUFANYA HUDUMA ZAKE KIDIJITALI”.♦️

♦️MBODO : “KIKAO CHENU KIJIKITE KUJADILI MWELEKEO WA POSTA KUFANYA HUDUMA ZAKE KIDIJITALI”.♦️

59056AB6 40B3 48CD AC01 62D6AF4D19D0 

 

 Na mwandishi wetu,Mwanza

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo ameliasa Baraza la Majadiliano la Shirika hilo lijikite kujadili mikakati ya kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za Posta kidijitali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja na wananchi kwa ujumla pamoja na kuongeza mapato.
 
Ameyasema hayo tarehe 9 Novemba, 2022 wakati akifungua kikao cha 34 cha Baraza la Majadiliano cha Shirika la Posta Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Adden Palace, Jijini Mwanza.
 
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Postamasta Mkuu amewaasa Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi na Wafanyakazi wa Shirika hilo kubadili mitazamo yao katika utendaji kwani kwa sasa wananchi wanataka kuhudumiwa wakiwa mahali walipo, hii ni kutokana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia na vionjo vya wateja kulingana na maendeleo ya kidijitali.
 
“Miaka 20 iliyopita sio kama sasa kwa sababu kwa sasa wananchi wanataka kuhudumiwa wakati wowote na mahali popote kwa kasi na weledi zaidi kwani wananchi wanataka kufuatwa mpaka walipo”. Akisisitiza Bw. Mbodo.  
 
Aidha Postamasta Mkuu ameeleza kuwa, Menejimenti ya Shirika la Posta kupitia mpango mkakati wake wa 8 wa Shirika hilo imedhamiria kuifanya Posta ya Kidijitali kwa Biashara Endelevu ili kuendana na mikakati na agenda mbalimbali za kitaifa na kimataifa katika kutoa huduma stahiki kulingana na mahitaji ya wateja.
 
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Majadiliano ndugu Bw. Omari M. Dibibi Amempongeza Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo kwa juhudi zake na maono ya kuifanya Posta kuwa ya kidijitali na pia amemuahidi kuunga mkono juhudi hizo za kimaendeleo zinazofanywa na Shirika ili kuleta matokeo chanya yenye tija kwa Shirika.
 
Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Mbaruku Makame ametumia nafasi hiyo kuwataka Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania kufuata misingi ya kazi na kuunga mkono maono ya Shirika yaliyomo kwenye mpango mkakati wa 8 kama ilivyofafanuliwa na Postamasta Mkuu wa Shirika hilo.
 
 
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano, 
Shirika la Posta Tanzania,

Picha zaidi za tukio hilo,

B336B87A 658E 4B29 88BC 7B871B2E702F

 1BB753BC 2DDE 491E 846F 99CC8DBB3D82

 10A9ABC7 523D 4E30 B38E DD3195733297

 8A78FE6F F8AD 4AEB A599 CFB7AB659521

 29E8B346 34D3 4865 8AF3 07C0876630F5

 B6BCDA6E 5851 4805 A32A DE0A90C10BF7

 F9C5DF17 7EE1 4A48 9211 2E47A5D7F8A4

 B8FED4EA F6BE 4B4D B463 03D2AAC0267D

 

 

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!