📌 SHIRIKA LA POSTA, LAWAKUMBUKA MASHUJAA WA VITA YA KWANZA YA DUNIA.

📌 SHIRIKA LA POSTA, LAWAKUMBUKA MASHUJAA WA VITA YA KWANZA YA DUNIA.

495FA20D 1778 4AF2 8E90 92D017E31058

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Posta Kimataifa, ndugu Elia Madulesi (wa pili kushoto) akipokea shada la maua kutoka kwa mwakilishi wa Balozi wa Uingereza Nchini Ndugu Rajabu Thabit, (wa pili kulia) wakati wa uwekaji wa shada hilo kwenye ofisi ya Posta Sokoine kama ishara ya kuwakumbuka baadhi ya wafanyakazi wa Posta na Simu waliokufa wakati wa Vita Kuu ya kwanza ya Dunia. Kushoto ni mwakilishi wa Jumuiya ya Mashujaa wa Uingereza Nchini, Ndugu David Sawe na kulia ni Mwakilishi wa Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Julius Chifungo.

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

Tarehe 13 Novemba 2022 Shirika la Posta Tanzania likiwakilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Posta Kimataifa, Ndugu Elia Madulesi kwa niaba ya Postamasta Mkuu, limeweka Shada la maua kwenye jengo la Posta ya Zamani (Sokoine) kama ishara ya kuwakumbuka baadhi ya Wafanyakazi wa Posta na Simu wa iliyokuwa Serikali ya kikoloni ya Ujerumani na Uingereza, waliokufa wakati wa Vita kuu ya Kwanza ya dunia.

Wafanyakazi hao waliokuwa wataalamu wa mifumo ya Mawasiliano ya Posta na simu, walihusika kama wadukuzi na watoa taarifa za vita, huku wakifanya kazi katika Jengo la Posta Sokoine ambalo ndilo lililokuwa Makao Makuu ya Posta na Simu ya Serikali za kikoloni katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Uwekaji huo wa mashada umehusisha baadhi ya Wafanyakazi kutoka Shirika la Posta Tanzania, wawakilishi kutoka Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Ujerumani, na Jumuiya ya Mashujaa wa Uingereza.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania .

 Picha zaidi za tukio hilo,

A3D7B004 376E 41BB BE66 FB5D1D85EFF0

 30124DBA D947 450E BD3A F677348370A8

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Posta Kimataifa, ndugu Elia Madulesi (wa pili kulia- mwenye suti ya bluu) akizungumza jambo wakati wa uwekaji wa shada la maua katika jengo la Posta Sokoine, Dar es Salaam.

 8BDDC820 901F 4F6F A6DA 68411F5D0B89 

 65BA411B B494 4093 953D 27BC26FF6084

 Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uingereza akipiga chombo cha muziki cha asili ya Uingereza wakati wa tukio la kuweka shada la maua kuwakumbuka baadhi ya wafanyakazi wa Posta na Simu waliokufa wakati wa Vita Kuu ya kwanza ya Dunia.

D9769326 6524 480C 9A68 12F48D2B0C77 

 D0244D08 5EAB 45C5 B501 EA00E4A4E0CA

 

 

 

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!