Shirika la Posta Tanzania (TPC) lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 19 ya mwaka 1993 na kuanza rasmi kutoa huduma zake mnamo tarehe 1 Januari, 1994 ikiwa na jukumu la kutoa huduma za ndani za kiposta na huduma za posta za kimataifa.
Shirika liko chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambayo ina jukumu la kusimamia, kutunga sheria, sera na miongozo mbalimbali kupitia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika.