JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

ZIARA YA M/KITI PAPU-POSTA DODOMA


Dodoma
18 Januari, 2023


ZIARA YA MWENYEKITI WA BARAZA LA UTAWALA UMOJA WA POSTA AFRIKA KATIKA OFISI ZA POSTA DODOMA

Mwenyekiti Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Posta Madagascar Richard Ranarison akiambatana na Katibu Mkuu Umoja huo Bw. Sifundo Chief Moyo wametembelea Ofisi za Shirika la Posta Tanzania mkoa wa Dodoma.

Ziara hiyo yenye lengo la kufahamu utendaji na kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika la Posta mkoani humo ilifanyika mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Posta Afrika yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Katika ziara yake Bw. Ranarison amepata nafasi ya kutembelea kituo cha Huduma Pamoja kinachotoa huduma mbalimbali za Serikali kilichopo katika ofisi hizo pamoja na kujionea mifumo mbalimbali ya Posta Tanzania inavyofanya kazi katika kufikisha huduma zake kwa wananchi.

Bw. Ranarison ameeleza kufurahishwa na ubunifu unaoendelea kufanywa na Shirika la Posta Tanzania na kupongeza juhudi zinazoendelea kufanyika katika kuboresha huduma za Posta nchini.

Wengine katika ziara hiyo ni Katibu Mkuu Msaidizi wa PAPU Bi. Jessica Ssengooba pamoja na Viongozi waandamizi kutoka PAPU 

Shirika la Posta Tanzania liliongozwa na Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma Bw. Ferdinand Kabyemelea pamoja na Viongozi waandamizi kutoka Shirika la Posta.
 

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA